MTU ALIE KUFA


 Mwili wa mtu ambaye aliwahi kusema: “Mimi ndiye mola wenu mkuu zaidi”… sasa umelala bila uhai kama ishara kwa wanadamu wote.


Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur’an:

“Basi leo tutakuokoa mwili wako ili uwe ni ishara kwa watakaokuja baada yako…”

(Surah Yunus 10:92)


Firauni ambaye alidhulumu, akakanusha haki, na kumpinga Mwenyezi Mungu, hakuhifadhiwa kama alama ya ukuu… bali kama onyo.


Haijalishi mtu ana nguvu kiasi gani, au anapanda juu kiasi gani, ukweli utashinda na kiburi kitaanguka.


Hili si historia tu. Huu ni ujumbe kwa kila kizazi:

👉 Tafakari

👉 Tubu

👉 Rudi kwa Allah kabla hajamaliza punzi yako


Yupo Mungu Mmoja tu aliye mpweke, hajazaa wala hajazaliwa, hafanani na yeyote yeye ni wa tangu ametukuka na mwenye nguvu.


Allah atupe mwisho mwema.🤲


#MUNGUMKUBWA

Comments

Popular posts from this blog

KIHUSU MUDATHIR

MPANZU SOMA HAPA.

USAJILI MPYA SOMA