KUHUSU MPHO MUPARANG.


 Taarifa Rasmi kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga SC 🔰


Leo naandika ujumbe huu mzito kwa moyo wa shukrani, heshima na majonzi kidogo, kumuaga mmoja wa watu muhimu sana katika mafanikio ya timu yetu katika misimu ya hivi karibuni — Mpho Muparang, Video Analyst wetu mpendwa.


Tangu ajiunge nasi, Mpho amekuwa zaidi ya mfanyakazi; amekuwa sehemu ya familia ya Yanga. Uwezo wake wa kuchambua kila sekunde ya mchezo, kutupa taarifa sahihi kuhusu wapinzani wetu, kutengeneza mbinu bora kupitia video na kusaidia benchi la ufundi kufanya maamuzi yaliyojaa ushahidi — umetufikisha mbali. Mchezo wa kisasa unahitaji akili kubwa nyuma ya pazia, na Mpho alikuwa moja ya silaha zetu kubwa kisayansi katika ushindi wetu mwingi.


Ni vigumu kuamini kuwa huu ni mwisho wa safari yetu pamoja, lakini kila mwisho ni mwanzo wa jambo jipya. Tunaamini anapoenda, ataendelea kuwa balozi mzuri wa Yanga na ataendelea kuliwakilisha bara la Afrika kwa weledi na maarifa yake makubwa ya kiufundi.


Kwa niaba ya uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji, na mashabiki wote wa Wananchi, ninamshukuru sana Mpho kwa mchango wake mkubwa. Milango ya Jangwani itakuwa wazi siku zote kwa mtu wa namna yako.


Asante kwa kila dakika, kila mchango na kila jasho ulilolitumikia klabu yetu. Tunakutakia kila la heri katika hatua yako inayofuata.


💚💛

#AsanteMpho #OnceGreenAlwaysGreen

 #YangaFamily

Comments

Popular posts from this blog

KIHUSU MUDATHIR

MPANZU SOMA HAPA.

USAJILI MPYA SOMA