Posts

Showing posts from March, 2026

MTU ALIE KUFA

Image
 Mwili wa mtu ambaye aliwahi kusema: “Mimi ndiye mola wenu mkuu zaidi”… sasa umelala bila uhai kama ishara kwa wanadamu wote. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur’an: “Basi leo tutakuokoa mwili wako ili uwe ni ishara kwa watakaokuja baada yako…” (Surah Yunus 10:92) Firauni ambaye alidhulumu, akakanusha haki, na kumpinga Mwenyezi Mungu, hakuhifadhiwa kama alama ya ukuu… bali kama onyo. Haijalishi mtu ana nguvu kiasi gani, au anapanda juu kiasi gani, ukweli utashinda na kiburi kitaanguka. Hili si historia tu. Huu ni ujumbe kwa kila kizazi: 👉 Tafakari 👉 Tubu 👉 Rudi kwa Allah kabla hajamaliza punzi yako Yupo Mungu Mmoja tu aliye mpweke, hajazaa wala hajazaliwa, hafanani na yeyote yeye ni wa tangu ametukuka na mwenye nguvu. Allah atupe mwisho mwema.🤲 #MUNGUMKUBWA

Alioa mwanamke asie pona jipu

Image
 Alipomuona kwa mara ya kwanza, hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa mke wake. Wengine walimwangalia kwa jicho la tofauti—si kwa sababu hakuwa mzuri, bali kwa sababu alikuwa na tatizo la kiafya lililomtesa kwa muda mrefu. Jipu lililokuwa mwilini mwake halikupona, na mara nyingi lilimletea maumivu makali na aibu mbele za watu. Lakini yeye alimwona tofauti. Hakumwona kama mgonjwa… alimwona kama mwanamke mwenye moyo wa upendo, mwenye utu, na mwenye thamani kubwa kuliko walivyodhani watu. Watu walimshangaa alipomtambulisha rasmi kuwa ndiye mwanamke aliyemchagua kuwa mke wake. Wengine walimcheka waziwazi. “Umeshindwa kupata mwanamke mzima?” walimuuliza kwa kejeli. Lakini yeye alitabasamu tu. “Nilichagua moyo wake, si mwili wake,” alijibu kwa utulivu. Baada ya ndoa, maisha hayakuwa rahisi. Kulikuwa na siku ambazo maumivu yalikuwa makali kiasi kwamba mke wake alishindwa hata kusimama. Siku hizo, mwanaume huyo hakuwahi kumwacha peke yake. Alimsaidia kwa kila kitu. Alimhudumia bila ...